Hakuna Misa Bila Ekaristi Takatifu

2025-06-22
Sherehe ya Mwili na Damu ya Bwana Wetu Yesu Kristo
Pd. Nicas Mrosso, OFMCap.
📖 Masomo ya Dominika

Somo la Kwanza: Mwa 14:18-20

Somo la Pili: 1Kor 11:23-26

Injili Lk 9:11-17

 

🕊️ Tafakari ya Neno

Utangulizi:

Ndugu wapendwa leo tunaadhimisha kwa namna ya pekee sherehe ya mwili na damu ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa kufuata agizo alilotoa yeye mwenyewe; “fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu” (Lk 22:19). Hivyo ni karamu ya duniani na mbinguni tunapoiadhimisha kwa mastahili na kushiriki kwa ibada.

 

Tafakari

Leo ndugu zangu wapendwa tunaadhimisha kwa namna ya kipekee kabisa Umungu wa Yesu katika maumbo ya Mkate na Divai. Ndio kilele cha maadhimisho yote ya kanisa. Tutazame kwa ufupi katekesi na majina ya Ekaristi Takatifu. Ekaristi Takatifu ni:

Hivyo tunapaswa kuiangalia Ekaristi Takatifu Kama tendo la shukrani na masifu kwa Baba, kumbukumbu ya sadaka ya Kristo na ya mwili wake, uwepo wa Kristo kwa uweza wa Neno lake na Roho wake.

     Ekaristi Takatifu na majitoleo ya kikuhani. Tunapewa picha hiyo kwa Mfalme Melkisedeki katika somo la 1. Ndio maana Ekaristi Takatifu na sadaka ya upadre vinafungamana. Na pia Ekaristi Takatifu ina muunganiko na matoleo ya vipaji na majitoleo yetu.

     Ekaristi inatuliza njaa na kiu ya karamu ya mbinguni. Yesu anawalisha makutano. Anatuliza njaa ambayo kwa macho ya kibinadamu na uwezo wa kibinadamu haikuwezekana. Tunaona wanafunzi wanamwaambia Yesu awaage makutano. Lakini Yesu anawalisha hataki waende bila kula. Yesu hapendi tushiriki misa takatifu bila kushiriki Ekaristi takatifu.

Basi tumwombe Yesu wa Ekaristi aingie katika maisha yetu na matendo yetu, ili tufungamane naye katika kutupenda na kupendana sisi kwa sisi ambayo maana ya Ekaristi kwetu. Amina.