Somo la Kwanza: Mwa 18:1-10
Somo la Pili: Kol 1:24-28
Somo la Injili
Lk 10:38-42
Ikawa katika kuenenda kwao Yesu aliingia katika kijiji kimoja; mwanamke mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.
Utangulizi:
Katika dominika ya tunaalikwa tujifunze namna ya kumkaribisha Mungu katika maisha yetu ya kila siku kwa karama zetu alizotujalia. Ukarimu, kuunganika na Kristo katika mateso yake na kutumikia kwa furaha kwa karama zetu ndizo dhamira za masomo yetu.
Somo la I:
Ukarimu wa Abrahamu unampelekea unampelekea kuwapokea malaika na kumpokea Mungu. Kisha Abrrahamu anatimiziwa ahadi yake. Bila kujua kama ni Mungu Abraham anawakaribisha kwa heshima malaika na anawatengenezea chakula bora na mahali pa kupumzika. Katika somo hili tunajifunza kwamba katika ukarimu wetu kwa wageni kwa wengine tunawapokea malaika bila kujua. tunakutana na Mungu bila kujua. Tuwe watu wa ukarimu.
Somo la II:
Katika somo la pili Paulo anatufundisha kuwa, ukarimu pia ni katika kushiriki mateso ya Kristo, kwa ajili ya wokovu kwa wengine. Kristo amekuwa mkarimu kwetu hata kiasi cha kutoa uhai wake kwa ajili yetu. Hakuna jambo kubwa tunaloweza kufanya liushinde huo ukarimu wa Kristo. Hivyo tunapopata tabu au shida au mateso kwa ajili yetu na kwa ajili yaw engine, tunashiriki mateso ya Kristo.
Injili:
Katika Injili tunakutana na simulizi la Martha na Maria. Wote wawili wanaonyesha ukarimu wao na karama yao kwa Yesu na kila mmoja anathaminiwa kwa Yesu. Yesu anathamini kile unachofanya. Ili hali ukifanye kwa moyo bila manung’uniko.
Yesu anatufundisha kuwa Chochote ulichonacho ama karama yako ni ya thamani kubwa sana. Martha na Maria wanatufundisha kuwa tunapojishughulisha na mambo ya Mungu, kwa sala na kwa ukarimu Mungu anapokea.
Kukaa miguuni pa Yesu ni ukarimu pia na baraka kwa maisha yetu. Tunajifunza namna ya kusikiliza na kutulia miguuni pa Yesu. Tuombe Mungu atujalie neema ya kuweza kutambua karama zetu na kuzitendea kazi bila manung,uniko.