Injili Luka 24:1 -1 2
Injili Luka 24:1 -1 2
Katika sherehe ya Pasaka tunaadhimisha kilele cha mafumbo ya ukombozi wetu. Maadhimisho yetu yote ya sala, ya liturujia hupata maana kutokana na sikukuu ya Pasaka.
Pasaka ndio utimilifu wa utume wa Yesu hapa duniani. Na ndio mwanzo mpya wa maisha ya Yesu ulimwenguni, na mwanzo mpya wa maisha ya ukombozi wa mwanadamu. Pasaka ni Ushindi: Kristo ameshinda alleluia alleluia! Baada ya Ijumaa Kuu, Waliomuua Yesu walifikiri wamemaliza kila kitu, walifikiri wamemaliza habari za Yesu. Kumbe la! Hakika Ndio mwanzo mpya wa uwepo wa Yesu katika maisha ya kanisa, katika maisha yetu. Masaomo ya leo yanatuthibitishia hilo: Somo la I: Kristo aliyeishi kati ya Wayahudi na akauwawa na Wayahudi ndiye anayeshi.
Petro anatoa ushuhuda wa ufufuko wa Yesu. Kwamba Yesu mliyemuuwa, amefufuka na anaishi ni Mzima. Ufufuko wa Yesu unamfanya Petro aliyemkana Yesu kuwa mpya, na Kutangaza habari zake kwa ujasiri. Ufufuko wa Yesu usikuache kama jana, uskubali kubaki vile vile. Somo la II: Kwa ufufuko wa Kristo, uhai wetu umefichwa ndani ya Kristo. Paulo anawaimarisha Wakolosai kwamba Masiah aliyesubiriwa na aliyeahidiwa, Mungu ametimiza ahadi hiyo katika Kristo. Ndiye Masiha aliyeaguliwa na kwa ufufuko ameketi Mkono wa kuume wa Mungu (Zab 1 1 0:1 ). Kristo ameketi Mkono wa Kuume na kuwafanya adui zake kuwa chini ya miguu yake. Adui wa kwanza aliyebatilishwa ni mauti. Injili: Ushuhuda wa kwanza wa ufufuko wa Yesu ni kaburi wazi. Mariamu Magdalene anatudhihirishia hilo, asubuhi na mapema anakuta kaburi li wazi. Jiwe kuondolewa kaburini si kwa nguvu ya kawaida kwani waliliweka kubwa ili kuzuia wanafunzi wake wasije kumwiba. Uthibitisho wa pili ni ule wa Petro na mwanafunzi mwingine. Wanaona sanda na leso peke yake. Na uthibitisho mwingine ni Yesu kuwatokea wanafunzi wake na wafuasi wengine. Huu ni uthibitisho wa kihistoria ya kwamba Yesu amefufuka kweli. Lakini swali ni Je, Ufufuko wa Yesu ni wa namna gani? Ni wa kibaologia, kama alivomfufu Larazo? Hapana! Wa lazaro uliitwa Resuscitation. Je Yesu ameingia katika hali ya mizimu/ghost? (kama baadhi ya tamaduni nyingi zinavyoamini mtu akifa anaingia kwa ulimwengu mizimu/spirits) Hapana!, licha ya kwamba anao uwezo wa kutokea katika hali ya roho.
Yesu ameingia kwenye maisha ya umungu na umilele ambao nasi tunatarajia mwisho wa nyakati. Ambao hata sisi ambao hatukumshuhudia akiwa hapa duniani tunaweza kumwona. Ufufuko wa Yesu ni: Maisha mapya: ufufuko wa Yesu ni kuingia katika maisha mapya, maisha ya umungu na ya umilele. Kuwekwa huru dhidi ya dhambi na mauti. Ushindi: Kwanza ushindi dhidi ya mauti. Pia ni kushinda giza, kuwa watu wa mwanga, watu wa nuru kama tulivyoona liturujia ya mwanga jana usiku. Kueneza habari njema ya Injili: Maria Magdalene anatufundisha hilo, amekuwa mmisionari wa kwanza wa habari njema ya matumaini. Kushinda magumu: wala Jiwe, wala walinzi hawakuweza kushinda nguvu ya ufufuko. Kwa Kristo Mfufuka hakuna linaloshindikana, mwamini yeye/ Trust Him, Mkabidhi hilo jiwe linalokushinda. Ufufuko wa Yesu ndio kiini cha imani yetu. Paulo anatuambia, Kristo asingefufuka kutoka wafu basi imani yetu ni bure (1 Kor 1 5:1 7) na hata kuhubiri kwetu kungekuwa bure (1 Kor 1 5:1 4).
Kristo amefufuka kweli Alleluia Alleluia!