Somo la Kwanza: Mdo 1:1-11
Somo la Pili: Efe 1:17-23
Injili: Mt 28:16-28
Somo la Kwanza: Mdo 1:1-11
Somo la Pili: Efe 1:17-23
Injili: Mt 28:16-28
Utangulizi
Leo tunaadhimisha sherehe ya Kupaa kwa Bwana. Ni takribani siku arobaini tangu tusherekee ushindi wa ufufuko wa Bwana. Ukuu wa ushindi huo unadhihirishwa kwa kupaa kwa Bwana. Yesu anadhihirisha ukuu wake kwa kuingia katika Muunganiko na Baba na kuonesha mamlaka ya Kristo mbinguni na duniani. Tumwombe Mungu atujaliwe kuinuliwa na nguvu za Kristo mfufuka.
Homilia
Kupaa kwa Yesu ni fumbo la imani yetu. Ni ushindi wa utukufu wa Yesu baada mateso, kifo na ufufuko. Ni Kufunguliwa mbingu kwa ajili yetu. Ni kuonesha muunganiko wa Yesu katika Umungu wake. Mamlaka ya Yesu Kristo mbinguni na duniani yanadhihirishwa.
Somo la I: Katika somo la kwanza tunaona wanafunzi wanamtazama Yesu Kristo akipaa kwenda kwa Baba. Licha ya Kwamba amekuwa akiwapa wosia bado wanapatwa na mshangao, na wasiwasi na kukosa matumaini. Lakini Malaika anawakumbusha kuwa Yesu huyo bado yupo nasi. Anakuja vile alivyoenda. Malaika anawapa ushuhuda wa ushindi wa Kristo dhidi ya dhambi dhidi ya mauti. Kupaa kwa Bwana sio kwamba tumeachwa yatima bali Kristo ameingia kwenye mamlaka yote, kwenye umungu wake, kwenye utukufu wake.
Katika somo hili tunajifunza kuwa watu wa matumaini na ujasiri. Kristo aliyefufuka anatupa matumainai kwamba kwa umungu wake anaingia katika muunganiko na Baba na sisi kama mwili wake.
Somo la II: Katika somo la pili Mtume Paulo anadhihirisha wazi kuwa, Kristo ameingia katika utukufu wake kwa kuungana na Baba na kwa kutushirikisha sisi pia kama viungo vya mwili wake. Anatuhimiza kabisa tutambue tumaini la mwito wake na utajiri wa utukufu wa urithi wake. Kwa kupaa kwake amedhihirisha huo utukufu kwetu. Kuketi kuume kwa baba kunadhihirisha kuwa ni kuhani wetu duniani na mbinguni. Hii inadhihisha maneno ya Mt. Augustino kuwa, alipaa kwa baba lakini bado yupo nasi kupitia kanisa. Kwa sala, sakramenti na kwa maadhimisho matakatifu.
Katika somo hili tunaitwa kama wanakanisa kushiriki utukufu wa Kristo kwa kuishi na kuihubiri Injili. Kupaa kwa Yesu ni kwamba anataka afanye kazi ndani yako. Mruhusu kwa utayari wako wa kupokea Injili na kuihubiri kwa wengine.
Injili: Katika somo la Injili Yesu anatupa jibu la maana ya kupaa. Kwamba ni kutambulishwa kwa mamlaka ya Yesu Mbinguni na duniani. Hivyo Yesu anadhihirisha ule ushindi wa ufufuko wa mamlaka yake. Yeye ni Bwana wa Mbingi na Nchi. Mbinguni yupo mkono wa kuume na duniani yupo nasi katika kanisa – ndani ya mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu. Baada ya kudhihirisha mamlaka hayo anatushirikisha na sisi, “enendeni” Tunashirikishwa mamlaka hayo kama wana kanisa kama Wakristo.
Hivyo ndugu zangu katika masomo Yetu tunajifunza kuwa;
Hivyo ndugu zangu tumwombe Bwana aliyepaa mbinguni adhihirishe nguvu zake ndani yetu nasi tuzitende kwa upendo na kwa kuihubiri injili. Atujalie kuwa viungo hai wa Mwili wake.