Somo la Kwanza: Mdo 1:1-11
Somo la Pili: Efe 1:17-23
Injili Lk 24:46-53
Somo la Kwanza: Mdo 1:1-11
Somo la Pili: Efe 1:17-23
Injili Lk 24:46-53
Utangulizi
Kwa juma zima tokea Dominika ya 6 tumekuwa tukisikia wosia wa Yesu kwa wanafunzi wake kwamba anaenda kwa Baba. Hali na picha tulioiona kwa wanafunzi wake ni ya kuwa na huzuni. Leo tunasikia tofauti kwamba Yesu anapoondoka mbele yao, wanafurahi. Ni furaha ya kutukuzwa kwa Yesu. Hivyo kupaa Bwana ni furaha kwetu kwa kuwa Yesu anakuja karibu zaidi nasi.
Homilia
Kupaa kwa Bwana inaonekana kana kwamba Yesu anakwenda mbali sana, sehemu ambapo hapafikiki ama panafikika kwa shida. Labda kwa kuwa tunasikia Yesu anapaa kwenda Mbingini, anachukuliwa juu mawinguni, anapaa juu kwa Baba. Fikra zetu zinaenda mbali kiasi cha mwisho wa Dunia. Lakini Kiuhalisia sivyo. Mzaburi alishatufunulia hili kuhusu kutukuzwa kwake (Zab 110:1), ataketi mkono wake wa kuume wa Mungu Baba, (pia Rum 8:34; Matt 26:64; Ebr 10:12, 1Pet 3:22). Yesu anayeketi kuume kwa Baba anatufikishia sala zetu kwa ukaribu zaidi na ndiye aliyepewa mamlaka juu yetu mwisho wa nyakati.
Somo la 1
Katika somo la kwanza la kitabu cha Matendo ya Mitume linatudhihirishia kwambakupaa kwa Bwana ni uwepo wa Mungu karibu zaidi katika maisha yetu.
Injili
Safari hiyo ya Yesu kuingia katika fumbo la Umungu ndiyo anayotuonyesha Mwinjili Luka kwamba Kupaa kwa Bwana sio safari ya Yesu kutoka katika maisha yetu. Yesu anaingia zaidi katika maisha yetu kwa fumbo la Umungu akiwa na nguvu na uwezo. Mateso kifo, ufufuko na kupaa kwake Yesu, ndio njia aliyoamua kutumia Mungu ya kuunganika kifumbo katika mwana wake.
Somo la II
Paulo anatuambia Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baada ya kumfufua katika wafu, amemweka Mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; Juu sana kuliko falme zote, kuliko mamlaka yote, kuliko nguvu zote, kuliko usultani wote. Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake. Tuna uhakika anatuona na anatusikia tumuitapo kwani ameingia kwenye hali ya Umungu. Kupaa kwa Bwana wetu Yesu Kristo Ni furaha kwetu kwamba, tunaye Bwana na mfalme aliyeketi kuume kwa Baba. Hakuna mamlaka, nguvu, ufalme, mtu, kitu, au chochote chenye uwezo wa kumshinda. Hata adui yetu shetani amewekwa chini ya miguu yake. Mkabidhi Yesu adui zako atawaweka chini ya miguu yake. Na tunapounganika naye, hakika adui zetu wanawekwa chini ya miguu yetu.